Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araqchi, kupitia ukurasa wake wa X, amezungumzia mazishi ya mashahidi Makamanda wa Kijeshi na Wanasayansi wa Iran, Watoto na Wanawake wasiokuwa na Hatia waliouawa na utawala haram wa Kizayuni.
Alisisitiza kwamba Taifa la Iran linaonesha mshikamano Umoja na ujasiri wake mbele ya ulimwengu mzima.
Araqchi alisema kuwa mamilioni ya watu waliojitokeza mitaani kuwaaga makamanda wa kijeshi, wanasayansi, na watoto waliouawa kwa kikatili ni ishara ya wazi ya Mshikamano na Umoja wa Kitaifa, na ni anguko kubwa la maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Alifafanua kuwa tofauti na utawala wa Kizayuni, Iran haitaficha hasara zake na inajivunia mashahidi wake kama vielelezo vya ujasiri. Kila afisa wa Kijeshi au Mwanasayansi wa Nyuklia anayeuliwa, kutakuwa na wengine mia moja nyuma yake walioko tayari kuchukua nafasi yake.
Mwishoni, alisisitiza kuwa taifa la Iran litasimama kidete dhidi ya yeyote anayejaribu kuliamulia mustakabali wake hadi tone la mwisho la damu.
Your Comment